Rais Emmanuel Macron aelekea Marekani
29 Novemba 2022Hatua hiyo ya kufufua juhudi za kidiplomasia ilisitishwa kutokana na janga la Covid-19.
Uhusiano kati ya marais hao wawili ulikuwa na mwanzo mbaya ambapo ilishuhudiwa rais Macron akimuita nyumbani kwa muda balozi wake nchini Marekani mwaka jana baada ya serikali ya Marekani kutangaza makubaliano ya kuiuzia Australia nyambizi zinazoendeshwa kwa nguvu za Nyuklia na kuuhujumu mkataba wa Ufaransa wa kutaka kuiuzia Autsralia nyambizi zinazotumia mafuta ya Diesel.
Viongozi hao wawili watakaa kwa mazungumzo mnamo siku ya alhamisi katika ikulu ya White House yatakajikita katika suala la mpango wa Nyuklia wa Iran, kuzidi kujiingiza kwa China katika eneo la nchi za bahari ya Pasifiki, na kuongezeka wasiwasi kuhusu usalama na uthabiti katika kanda ya Sahel barani Afrika.
Aidha agenda kuu zaidi katika mazungumzo yao ni Ukraine.
Rais Macron ameongozana kwenye ujumbe wake na mawaziri wa mambo ya nje,Ulinzi na fedha pamoja na viongozi wa kibiashara na wanaanga.