1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Felix Tshisekedi kuapishwa Jumamosi

19 Januari 2024

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa kesho Jumamosi kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa pili.

https://p.dw.com/p/4bTDT
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi
Rais Felix Tshisekedi ataapishwa Jumamosi 20.1.2024 baada ya kushinda uchaguzi wa Disemba 20, 2023 ambao hata hivyo unapingwa na upinzaniPicha: Pool Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance

Hafla ya kuapishwa kwake inafanyika mjini Kinshasa chini ya kiwingu cha vuguvugu la upinzani linalopinga ushindi wake.

Rais Tshisekedi atakula kiapo mbele ya Mahakama ya Katiba ili kuiongoza tena Kongo kwa miaka mingine mitano.

Serge Tshibangu, mwakilishi mkuu wa rais Tshisekedi amesema kuwa marais 18 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Pia wako makamu wa rais wawili, pamoja na marais wa zamani wanne.

Kwa mujibu wa Tshibangu wawakilishi wa ngazi za juu wa marais kutoka nchi za Ulaya na Marekani pia wamethibitisha kuhudhuria sherehe hizo. 

Hata hivyo upinzani unaendelea kudai uchaguzi huo uliompa usdhini Tschisekedi siyo halali na matokeo yake yanafaa kufutwa.