Rais Hugo Chavez ataka CNN ichunguzwe
29 Novemba 2007Matangazo
Rais Hugo Chavez wa Venezuela anataka shirika la habari la CNN lichunguzwe akidai linataka auwawawe.
Rais Chavez amesema hayo baada ya kituo cha televisheni ya CNN kinachotangaza kwa lugha ya kihispania kuonyesha picha yake kando ya kichwa cha maneno yalioyouliza, ´Ni nani aliyemuua mwanamume huyu.´
CNN imeomba radhi kwa mkanganyiko wa kiufundi ikisema maneno hayo yalihusu habari ya kuuwawa mchezaji wa timu ya Redskins, Sean Taylor, aliyepigwa risasi wiki hi nyumbani kwake huko Florida nchini Marekani.
Rais Hugo Chavez anataka uchunguzi ufanywe kwa kuwa ilionekana kama mwito wa kumuua rais nchini Venezuela.