1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Joe Biden "Ninataka kumalizia kazi niliyoianza."

12 Julai 2024

Rais Joe Biden wa Marekani ameutumia mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi kutetea sera zake za ndani na za kigeni na kupuuzilia mbali maswali kuhusiana na uwezo wake wa kuongoza kwa miaka minne mingine.

https://p.dw.com/p/4iCDa
Maadhimisho ya miaka 75 ya NATO, Washington
Rais Joe Biden wa Marekani akiwa kwenye mkutano wa kilele wa miaka 75 ya Jumuiya ya NATO mjini Washington, Julai 9, 2024Picha: REUTERS

Rais Biden amesisitiza wakati akiufunga mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami, NATO kwamba haongozi kwa maslahi yake na ndio maana ataendelea ili kukamilisha kazi aliyoianza, licha ya miito inayoongezeka ya kumtaka asigombee tena kutokana na wasiwasi juu ya uwezo wake.

Kwenye mkutano huo uliohitimisha kusanyiko la NATO iliyokuwa ikiadhimisha miaka 75, Biden alisema ataendelea kuisaidia Ukraine kijeshi baada ya mataifa wanachama wa jumuiya hiyo kuonyesha msimamo kama huo miaka miwili na nusu tangu Urusi ilipovamia Ukraine.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine licha ya kushukuru kwa misada hiyo aliwaomba washirika wa NATO kuondoa vizuizi vya namna jeshi lake linavyoweza kutumia silaha wanazosaidiwa na jumuiya hiyo ili kushambulia ndani ya Urusi.