1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Rais Macron kuidhinisha kujiuzulu serikali ya Ufaransa

16 Julai 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatazamiwa hivi leo kuidhinisha hatua ya kujiuzulu kwa serikali lakini anatarajiwa pia kumuomba Waziri Mkuu Gabriel Attal kusalia katika nafasi yake kwa muda.

https://p.dw.com/p/4iNe6
Serikali ya Ufaransa yajiuzulu
Rais Macron atamuomba waziri mkuu kubakia katika wadhifa wake kwa mudaPicha: Ruffer/Caro/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatazamiwa hivi leo kuidhinisha hatua ya kujiuzulu kwa serikali lakini anatarajiwa pia kumuomba Waziri Mkuu Gabriel Attal kusalia katika nafasi yake kwa muda.

Soma pia: Bunge jipya ya Ufaransa kukutana Alhamisi wiki hii

Siasa za Ufaransa zimekuwa katika hali ya sintofahamu tangu ulipofanyika uchaguzi wa mapema wa Bunge mwezi huu, ulioupa ushindi muungano wa siasa za mrengo wa kushoto wa New Popular Front.

Hata hivyo hakuna muungano wowote uliopata wingi wa kura ili kulidhibiti Bunge na hadi sasa miungano hiyo bado inataabika kumpata mrithi wa Waziri mkuu wa sasa Gabriel Attal.