Rais Paul Kagame wa Rwanda azuru Tanzania
27 Aprili 2023Matangazo
Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Tanzania tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipochukua wadhifa huo baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.
Rais Samia na Kagame wamekuwa na mazungumzo ikulu jijiji Dar es Salaam na kila mmoja amedokeza umuhimu wa kudumisha uhusiano mwema.
Rwanda imekuwa ikitegemea bandari ya Dar es Salaam kwa kusafirisha mizigo yake kutoka ng'ambo. Hadi mwaka 2021 Rwanda ilikuwa ikisafirisha tani milioni 1.366 kupitia bandari hiyo.
Moja ya malengo ya ziara ya Rais Kagame ni kuimarisha ushirikiano kupitia bandari hiyo ambayo imekuwa ikifanyiwa maboresho ili kukidhi mahitaji ya nchi jirani zinazoitegemea.