1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin akutana na Spika wa Bunge la Tanzania

11 Julai 2024

Rais wa Urusi, Vladmir Putin amefanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson wakati wa Mkutano wa Wabunge wa kundi la mataifa ya BRICS.

https://p.dw.com/p/4iBgN
 Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson.Picha: Ericky Boniphace

Viongozi hao wamezungumzia kuhusu uhusiano na ushirikiano wa BRICS. Putin amesema amemkaribisha mwakilishi wa Afrika kutoka Tanzania, nchi inayoinukia kiuchumi, ambaye sasa anaongoza shirika linaloheshimika kimataifa. 

Soma pia:

Spika Ackson pia amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Baraza la Shirikisho la Urusi, Valentina Matvienko kwenye mji wa St. Petersburg, Urusi. Spika huyo wa Tanzania yuko nchini Urusi kuhudhuria Mkutano wa Mabunge ya BRICS unaofanyika leo na kesho.