UchumiUrusi
Putin: Urusi bado ni mshirika muhimu kibiashara ulimwenguni
8 Juni 2024Matangazo
Putin amesema hayo jana Ijumaa kwenye Jukwaa la 27 la Kimataifa la Uchumi, SPIEF, mjini St. Petesburg na kuongeza kuwa Urusi ni miongoni mwa mataifa vinara kiuchumi, mbele ya Ujerumani akiangazia takwimu zinazozingatia uwezo wa manunuzi.
Kwenye hotuba mbele ya mamia ya wahudhuriaji, Putin alitoa wito wa kutanua ushirikiano katika masuala ya teknolojia na kutangaza matarajio yenye lengo la kuvutia wawekezaji zaidi kutoka nje.
Mataifa ya magharibi yameiwekea Urusi msururu wa vikwazo baada ya kuivamia Ukraine miaka miwili iliyopita.
Tangu kuwekwa kwa vizuizi hivyo vya kibiashara, Urusi imegeukia washirika wapya na hususan China, lakini pia India, Afrika na Amerika ya Kusini.