Rais Ruto awaomba wapinzani kutoa nafasi kwa mazungumzo
17 Aprili 2023Maelfu walishiriki katika maandamano ya siku tatu katika wiki mbili mwishoni mwa mwezi Machi yaliyogubikwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.
Maandamano hayo kwa kiasi fulani yanatokana na shutuma za udanganyifu katika uchaguzi wa urais wa Agosti ambapo Ruto alimshinda Raila Odinga kwa kura chache sana.
Siku ya Alhamisi, Odinga alisema upinzani utaanza tena maandamano baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani wa Waislamu, ili kuendana na mazungumzo kati yake na serikali.
Soma pia: Odinga asitisha maandamano yaliyoitikisa serikali ya Kenya
Muungano tawala wa Ruto umesema kura hiyo ilikuwa ya haki, ukatetea rekodi yake ya kiuchumi na kutaka maandamano hayo kukoma, ukisema yanatia shaka uaminifu wa upinzani kushiriki katika mazungumzo hayo.
"Kwanini tusitafute tunachotaka sisi viongozi bila fujo, uharibifu wa mali, ili tusikilize madai ya wananchi, huku tukijadili tunachotaka?" Ruto alisema.
Muungano wa Azimio La Umoja wa Odinga na Muungano wa Ruto wa Kenya Kwanza haikubaliani kuhusu maudhui ya mazungumzo hayo na ni nani anafaa kuyaongoza.
Kenya Kwanza inataka mazungumzo hayo kuhusisha wabunge pekee na kujadili uteuzi wa maafisa wa uchaguzi pekee.
Azimio inasema wengine wanapaswa kushiriki na mazungumzo hayo pia yanapaswa kupitia uchaguzi wa 2022 na kujadili hatua za kukabiliana na gharama ya maisha.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza Jumanne, kiongozi wa wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot alisema Jumamosi.
Soma pia: Afisa wa polisi auawa katika maandamano ya Kenya
Mwishoni mwa Machi, Odinga alisimamisha maandamano baada ya kuombwa na Ruto, lakini alirudia wito wake wa maandamano katika mkutano wa hadhara jijini Nairobi siku ya Jumapili.
"Ikiwa hatutasikia kutoka kwa Ruto wiki ijayo, baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunarudi mitaani," alisema odinga.
Chanzo: RTRE