Rais Samia Suluhu akutana na vyama vya siasa
3 Januari 2023Mkutano huo ni mwendelezo wa majadiliano ya ngazi ya juu yaliyoanzishwa na rais Samia tangu alipoingia madarakani mwaka 2021, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA ambacho mara zote kimekuwa kikikosoa mienendo ya serikali hasa linapokuja suala la democrasia.
Miongoni mwa hoja ambazo zinatarajiwa kuchukua muelekeo mpya baada ya majadiliano hayo , ni pamoja na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, marekebisho ya katiba pamoja na sheria kandamizi ambazo zinaongoza shughuli za vyama vya siasa.
Kwa takriban miaka mitano, vyama vya upinzanni nchini humo vimekuwa vikilalamika kukandamizwa na dola, hatua inayotajwa kuzorotesha ushiriki kamili wa shughuli za kidemocrasia katika taifa hilo la Afrika mashariki.