1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Trump kutoa tamko muhimu

Sekione Kitojo
27 Oktoba 2019

Kwa  mujibu  wa  msemaji  wa  Ikulu  ya  Marekani  Hogan Gidley rais wa  Donald Trump anapanga kutoa kile  kinachoelezwa kuwa  ni taarifa muhimu  leo Jumapili(27.10.2019)

https://p.dw.com/p/3S0hQ
Donald Trump
Picha: picture-alliance/dpa/AP/E. Vucci

Gidley hakutoa  taarifa  zaidi, na  haikuwa  wazi  kuhusu  mada itakayokuwa  katika  taarifa  hiyo  ya  Trump.

Rais ametoa  ishara  hapo  mapema  kuwa kuna  kitu muhimu anachotaka  kuzungumza  wakati  alipoandika  katika  ukurasa wa Twitter bila  kutoa  maelezo kwamba, "kuna kitu  kikubwa  kimetokea !"

USA Texas Wahlkampf Präsident Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump kutoa tamko muhimu Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Harnik

Trump  amekuwa  akikerwa  na  vyombo  vya  habari  vya  Marekani kutoa  umuhimu  mkubwa  kwa  uchunguzi  unaoongozwa  na chama cha  Democraitc  wa  kutaka  ashitakiwe, uchunguzi  ambao  anauita wa  kumtafuta  mchawi  ulio kinyume  na  sheria.

Pia amekabiliana  na  ukosoaji  mkubwa  kutoka  kwa  wanachama wa  chama  chake  cha  Republican  pamoja  na  Wademocrat pia kwa  uamuzi  wake  wa  kuvitoa  vikosi  vya  jeshi  la  Marekani kutoka  kaskazini  mashariki  mwa  Syria, hali  iliyoruhusu Uturuki kuwashambulia  Wakurdi  ambao  ni  washirika  wa  Marekani.

US-Präsident Trump begrüßt den polnischen Präsidenten Duda im Weißen Haus in Washington
Rais Trump(kulia) katika chumba cha mapokezi ya wanadiplomasia Picha: Reuters/K. Lamarque

Trump alitarajiwa  kutoa  taarifa  hiyo  katika  chumba  maalum  cha mapokezi  ya  wanadiplomasia  katika  Ikulu  ya  White House, chumba ambacho  amekuwa  akikitumia  kutoa  matamshi  kadhaa muhimu.

Ni  wiki  iliyopita  tu alitumia  chumba  hicho  kutangaza  kuwa usitishaji  mapigano  kati ya  Uturuki  na  Wakurdi wameanza.