1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin "Ukraine lazima ikubaline na masharti yetu"

5 Julai 2024

Rais Vladmir Putin wa Urusi amesema hawezi kutangaza kusitisha vita nchini Ukraine bila ya serikali ya mjini Kyiv kufikia masharti ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4huEf
Saint Petersburg 2024 | Rais Vladimir Putin akizungumza kwenye SPIEF
Rais wa Urusi Vladimir Putin akihutubia kongamano la kimataifa la uchumi la St. Petersburg International Economic Forum, SPIEF Juni 1, 2024 Picha: Anton Vaganov/REUTERS

Putin amesema Ukraine inaweza kutumia nafasi ya usitishaji vita kujihami kwa mashambulizi mapya na hiyo ndiyo sababu kunabidi kwanza kufanyike mazungumzo ya kupata suluhisho endelevu.

Kiongozi huyo wa Urusi aliyasema hayo jana Alhamisi huku pia akigusia makubaliano yaliyofikiwa huko nyuma kuhusu vita hivyo vya Ukraine ambayo yaliishia kutupiliwa mbali.

Mtazamo wa Putin umekuja katika wakati ambapo viongozi wa Umoja wa Ulaya jana walizungumzia wasiwasi wao kuhusu tetesi kwamba waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban anayeshikilia uongozi wa Umoja huo kwa sasa, anajiandaa kwenda Moscow.

Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel amesema Orban hana mamlaka ya kuchukua hatua hiyo.Michel amesema Urusi ni mchokozi na Ukraine ni muhanga kwa hivyo hakuna mazungumzo kuhusu Ukraine yanayoweza kufanywa bila ya Ukraine kuwepo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW