Rais wa Bulgaria aitisha uchaguzi wa bunge wa mapema
27 Agosti 2024Rais wa Bulgraia ameitisha uchaguzi wa mapema wa bunge,mwezi Oktoba katika hatua nyingine ya juhudi za kujaribu kuuondowa mkwamo wa kisiasa na matatizo ya kiuchumi yanayolikabili taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Nato na Umoja wa Ulaya.
Rais Rumen Rade ametangaza kwamba uchaguzi utafanyika Oktoba 27,ukiwa ni uchaguzi wa saba kuitishwa nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu.
Soma: Bulgaria yanapiga kura uchaguzi wa tano katika miaka miwili
Pamoja na hatua hiyo, pia amemteuwa tena Dimitar Glavchev kuiongoza serikali ya mpito hadi utakapofanyika uchaguzi.Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwezi Juni na ulishindwa kutowa mshindi wa moja kwa moja. Bulgaria nchi ya wakaazi milioni 6.7 imekuwa ikiandamwa na misukosuko ya kisiasa tangu mwaka 2020 baada ya kuzuka maandamano makubwa ya kuwapinga wanasiasa mafisadi.