1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi: Uhusiano kari ya China na Marekani ni muhimu kwa dunia

9 Oktoba 2023

Rais wa China Xi Jinping amesema uhusiano kati ya nchi yake na Marekani utakuwa na uzito katika mustakabal wa binadamu.

https://p.dw.com/p/4XJVi
Indonesien G20 Joe Biden und Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Joe BidenPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Rais Xi alisema hayo alipokutana na kiongozi wa baraza la seneti la Marekani Chuck Schumer mjini Beijing.

Schumer ni kiongozi mwengine mwandamizi wa Marekani anayefanya ziara nchini China wakati ambapo Marekani inajaribu kupunguza mivutano na China.

Rais Xi Jinping amesema jinsi China na Marekanizitakavyohusiana katika muktadha wa mabadiliko yanayotukia duniani ndivyo zitakavyouelekeza mustakabal wa dunia.

Soma pia:Biden: Kuna uwezekano wa kukutana na Rais wa China mwezi ujao

Kwa upande wake kiongozi wa wachache kwenye seneti ya Marekani Chuck Schumer amesema Marekani na China kwa pamoja zitaujenga mustakabal wa dunia.

Schumer amesema nchi hizo zinapaswa kuundeleza uhusiano wao kwa njia ya busara.

Pia amesema kusisitiza  masuala ya haki za binadamu ni muhimu na amesikitishwa na msimamo wa China juu ya mogogoro wa mashariki ya kati.

China imetoa wito kwa Wapalestinana na Israel kuwa watulivu badala ya kulaani mashambulio ya Hamas.