Rais wa Comoro asifu amani kabla uchaguzi wa Jumapili
10 Januari 2024Rais Azali Asumani amesifu rekodi yake ya kudumisha amani na kujenga barabara na hospitali katika nchi hiyo inayokabiliwa na umasikini. Wapiga kura kiasi 340,000 wanatarajiwa kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura kumchagua rais mpya katika uchaguzi ambao wagombea sita wanawania kiti cha urais.
Upinzani umegawika kati ya wale wanaotaka uchaguzi na wale wanaotaka uchaguzi huo ususiwe, hali inayoiweka kambi ya rais Azali Assoumani kuwa na matumaini makubwa ya kushinda katika duru ya kwanza ya upigaji kura.
Soma pia: Rais wa zamani wa Comoro Ahmed Sambi afungwa maisha kwa uhaini
Rais Assoumani, mwenye umri wa miaka 65 na ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ameitawala Comoro kwa mkono wa chuma na wapinzani wake wengi wametupwa gerezani au kulazimika kwenda uhamishoni.