Rais wa Haiti Jovenel Moise auawa
7 Julai 2021Matangazo
Mke wa rais Martine Moise amelazwa hospitalini kufuatia shamblio hilo lililofanyika Jumanne jioni, amesema waziri mkuu huyo wa muda Claude Joseph, kulaani kile alichokiita kitendo cha chuki, na unyama.
Taifa hilo lenye wakaazi milioni 11 limezidi kukosa utulivu na kuwa lenye chuki chini ya utawala wa Moise. Madhila yake ya kiuchiúmi, kisiasa na kijamii yameongezeka huku vurugu za magenge zikishika kasi hasa katika mji mkuu Port-au-Prince.
Mfumuko wa bei umeongezeka pakubwa katika taifa ambako asilimia 60 ya wakaazi wanapata chini ya dola mbili kwa siku. Moise aliekuwa na umri wa miaka 53, amekuwa akitawala kwa amri ya rais kwa zaidi ya miaka miwili, baada ya nchi hiyo kushindwa kufanya uchaguzi, hatua iliyopelekea kuvunjwa bunge.