SiasaUrusi
Ursula von der Leyen aanza ziara kuelekea Amerika Kusini
12 Juni 2023Matangazo
Von der Leyen atakutana na marais wa Brazil, Argentina, Chile na Mexico, na ajenda kuu itakuwa makubaliano ya biashara yaliyoanza mwaka 2019 na mataifa hayo lakini yalisitishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na wasiwasi juu ya ukataji miti katika msitu wa Amazon.
Umoja wa Ulaya umekuwa ukitafuta washirika wa kibiashara
Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, Umoja wa Ulaya umekuwa ukitafuta washirika wengine wa kibiashara wanaoweza kuwapatia madini muhimu yanayohitajika ili kufanikisha wakati wa mpito kuelekea matumizi ya nishati safi na pia kupunguza utegemezi wake kwa taifa la China.