1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Indonesia kuhudhuria mkutano wa BRICS Afrika Kusini

21 Agosti 2023

Rais wa Indonesia Joko Widodo ameondoka kuelekea Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi uliwenguni - BRICS utakaofanyika siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/4VNTQ
Indonesien ASEAN Gipfel Joko Widodo
Picha: Indonesian Presidency

Widodo atahudhuria mkutano huo huku kukiwa na minon'gono ya iwapo taifa lake huenda likajiunga na kundi hilo na kuwa mwanachama wake, lakini mwenyewe amesema serikali yake haijaamua kama itataka kujiunga na BRICS.  

BRICS yajadili uwezekano wa kujitanua na kujumuisha nchi zinazosafirisha mafuta

Mkutano huo wa siku tatu unaohudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama Brazil, Urusi , India, China na Afrika Kusini unanuiwa kuzuwia utawala wa kiuchumi wa mataifa ya Magharibi duniani. 

Hii ni ziara ya kwanza ya Widodo barani Afrika kama kiongozi wa taifa lililo na uchumi mkubwa Kusini Mashariki mwa Asia. Baada ya mkutano huo wa BRICS Widodo atazitembelea pia Kenya, Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.