1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran awasili Syria katika ziara yake ya kwanza

3 Mei 2023

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi amewasili Damascus katika ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Iran tangu vilipozuka vita vya Syria mwaka 2011

https://p.dw.com/p/4Qpk2
Syrien l Irans Präsident Raisi zum Staatsbesuch in Syrien
Picha: Omar Sanadiki/AP/dpa/picture alliance

Raisi amekutana na Rais wa Syria BAshar al-Assad katika juhudi za kuiamrisha ushirikiano kati ya washirika hao wawili.

Iran imekuwa ikiiunga mkono serikali ya Assad na imetoa msaada wa kijeshi kwa vikosi vyake vinavyopambana na waasi wanaojaribu kumuondoa madarakani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Amir Abdollahian amesema umuhimu wa ziara hiyo, pamoja na mwelekeo wake wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi, ni kudhihirisha ushindi wa dhamira ya kisiasa ya upinzani na mafanikio ya diplomasia ya utawala katika kukamilisha mchakato wa muunganiko wa kikanda.

Rais wa mwisho wa Iran kuizuru Syria, alikuwa Mahmoud Ahmadinejad mwaka 2010.