1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kongo afungua njia ya kuachiwa mwandishi Bujakera

24 Februari 2024

Mawakili wa mwandishi habari aliyeko kizuizini Stanis Bujakera wamesema wamewasilisha ombi jipya la kuachiwa kwake.

https://p.dw.com/p/4cpVJ
Maandamano ya waandishi habari wa Kongo kushinikiza kuachiwa kwa mwandishi habari aliye kizuizini Stanis Bujakera.
Maandamano ya waandishi habari wa Kongo kushinikiza kuachiwa kwa mwandishi habari aliye kizuizini Stanis Bujakera.Picha: Paul Lorgerie/DW

Hii ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kusema kuwa mwandishi huyo ni mwathiriwa wa mfumo dhaifu wa utoaji haki.

Mwandishi huyo wa jarida la Jeune Afrique na shirika la habari la Reuters, amekuwa kizuizini tangu Septemba 8 kuhusiana na makala iliyohoji uhusika wa intelijensia ya kijeshi katika mauaji ya kiongozi mmoja wa upinzani.

Katika kikao cha waandishi habari Alhamisi usiku, Rais Tshisekedi alikosoa kile alichokiita kucheleweshwa makusudi kwa kesi hiyo na kusema ameamua kujiingiza katika suala hilo na kuahidi kuchukua hatua inayostahili kuchukuliwa.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, wakala wa Bujakera Jean-Marie Kabengela amesema kumekuwa na hatua iliyopigwa katika kesi hiyo.