SiasaKorea Kusini
Rais wa Korea Kusini afanya ziara nchini Ukraine
15 Julai 2023Matangazo
Ziara hiyo ya kushtukiza imetangazwa leo na ofisi ya rais ya Korea Kusini na imefanyika baada ya Rais Yoon kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wa wiki iliyopita. Katika mkutano huo Yoon alionesha mshikamano na Ukraine na kutafuta njia za kuisaidia kwenye mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Korea Kusini yajiandaa kuipelekea Kyiv vifaa vya kutegua mabomu
Mapema wiki hii, Rais huyo wa Korea Kusini alisema kuwa serikali yake ilikuwa ikijiandaa kuipelekea Kyiv vifaa vya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini na magari ya kubebea wagonjwa baada ya kuombwa na Ukraine. Awali wawili hao walipokutana mwezi Mei, Zelensky alimuomba Yoon kuongeza msaada wa kijeshi.