Rais wa Moldova: Urusi ilipanga njama ya kuuangusha uongozi
13 Februari 2023Sandu amesema hatua hiyo ya Urusi inalenga kuizuia nchi yake isijiunga na Umoja wa Ulaya na kutumia taifa hilo dogo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Kulingana na Sandu, mpango unawahusisha raia wa Urusi, wa Montenegro, Belarus na Serbia na kuwawezesha kuingia Moldova kujaribu kuchochea maandamano katika jaribio la kubadilisha serikali rasmi na serikali haramu inayodhibitiwa na shirikisho la Urusi.
Sandu ametoa madai hayo baada yar ais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kusema wiki iliyopita kuwa nchi yake imegundua mpango wa kijaasussi wa Urusi wa kutaka kusababisha vurugu Moldova.
Mara kadhaa, Sandu ambaye nchi yake inapakana na Ukraine ameelezea wasiwasi wake kuhusu nia ya Urusi kuelekea jamhuri hiyo ya iliyokuwa chini ya Umoja wa kisoviet kuhusiana na uwepo wa vikosi vya Urusi katika jimbo lililojitenga la Transdniestria.