Kaimu rais Mokhber ahutubia bunge la Iran kwa mara ya kwanza
27 Mei 2024Kaimu Rais wa Iran Mohammad Mokhber amelihutubia bunge jipya la nchi hiyo, katika hotuba yake ya kwanza kwa umma tangu tukio la wiki iliyopita la kuanguka kwa helikopta lililosababisha kifo cha mtangulizi wake Ebrahim Raisi na maafisa wengine saba serikalini.
Katika hotuba yake, Mokhber amemsifu Raisi kwa muda aliokuwa afisini akisema Iran iliongeza uzalishaji wa mafuta wakati wa uongozi wake na kufikia mapipa milioni 3.6 kwa siku.
Kaimu huyo rais vile vile amesema uchumi wa nchi hiyo haukuyumba chini ya Raisi wakati nchi hiyo ilipozishambulia kijeshi Irak, Israel na Pakistan.
Hotuba yake hii inakuja wakati ambapo Iran inajiandaa kwa uchaguzi wa rais ili kulijaza pengo lililoachwa na Raisi.
Uchaguzi huo utafanyika Juni 28 na Mokhber huenda akajitosa katika kinyang'anyiro hicho pamoja na wengine.