1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Rais wa Nigeria akabidhiwa mikoba ya ECOWAS

10 Julai 2023

Wakuu wa nchi wa mataifa ya Afrika Magharibi wamemchagua Rais Bola Tinubu wa Nigeria kuongoza Jumuiya ya kikanda ya ECOWAS kwa muhula wa mwaka mmoja.

https://p.dw.com/p/4TfN2
Nigeria, Bola Ahmed Tinubu
Rais Bola Tinubu wa NigeriaPicha: Sunday Aghaeze/AP Photo/picture alliance

Wakuu wa nchi wa mataifa ya Afrika Magharibi hapo jana walimchagua Rais Bola Tinubu wa Nigeria kuongoza Jumuiya ya kikanda ya ECOWAS kwa muhula wa mwaka mmoja akichukua mikoba kutoka kwa kiongozi wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa uenyekiti, Tinubu amesema demokrasia inasalia kuwa mfumo bora wa kuunda serikali licha ya kukrii kuwa ni mfumo mgumu kuusimamia.

Amesema kanda ya Ecowas ni lazima iwe mfano barani Afrika na duniani kwa demokrasia na kwamba eneo hilo halitakubali kuona mapinduzi ya kijeshi ya kila wakati. Nchi tatu wanachama wa Ecowas, za Mali, Burkina na Guineazimeshuhudia awamu tano za Mapinduzi ya kijeshi tangu mwaka 2020. 

Mkuu wa kamisheni ya Jumuiya ya Ecowas Omar Alieu Touray aliutumia mkutano huo uliofanyika jana mjini Bissau kuwarai watawala wa kijeshi kwenye mataifa hayo matatu kuheshimu muda uliowekwa wa kurejesha utawala mikononi wa serikali za kiraia. Ameonya kuwa iwapo hilo halitazingstiwa vikwazo vikali vya kiuchumi vitawekwa dhidi ya tawala hizo.