Rais wa Poland aitaka Ujerumani iwalipe fidia ya vita
1 Septemba 2024Rais Duda amerejelea madai hayo leo katika hotuba yake ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 85 tangu Ujerumani chini ya utawala wa manazi ilipoivamia Poland.
Akizungumza katika mji mdogo wa Wielu uliokuwa wakati huo karibu na mpaka kati ya Ujerumani na Poland, Duda amesema suala la kusamehe na kukiri makosa ni kitu kimoja lakini kulipa fidia ni suala jingine.Duda ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa chama cha kihafidhina PiS kilichowahi kuiongoza seriikali.
Wakati huo serikali ya PiS ilikuwa na mahusiano mabaya na Ujerumani ambapo Poland iliishinikiza Ujerumani iilipe fidia ya jumla ya Euro Trilioni 1.3. Serikali ya sasa inayoongozwa na waziri mkuu Donald Tusk ambayo ina maelewano na serikali ya mjini Berlin,iko kwenye mazungumzo na Ujerumani yaliyoanza mwezi Julai,juu ya suala hilo la fidia.