1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Poland azuru Ukraine kuelekea mkutano wa NATO

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Rais wa Poland Andrzej Duda amesisitiza haja ya mshikamano na Ukraine wakati alipotembelea nchi hiyo kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya kujihami NATO utakaofanyika nchini Lithuania mapema wiki hii..

https://p.dw.com/p/4Tdk7
Ukraine |  Andrzej Duda  Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Poland Andrzej Duda na mwenyeji wake Volodymyr ZelenskiyPicha: Alina Smutko/REUTERS

Rais wa Poland Andrzej Duda  amesisitiza haja ya mshikamano na Ukraine wakati alipotembelea nchi hiyo kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya kujihami NATO. Duda ameyasema hayo leo Jumapili wakati alipotembelea mji wa magharibi mwa Ukraine wa Lutsk akiwa na mwenyeji wake Rais Volodmyr Zelensky.Ukraine lazima iamue mustakabali wake yenyewe: Duda

Marais hao wawili walikutana katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya Wapoland yaliyofanywa na Waukraine wakati wa vita vya pili vya dunia. Mauaji hayo yamekuwa chanzo cha mvutano kati ya mataifa hayo washirika. Wanahistoria wanasema mauaji hayo ya Volhynia yalisababisha maelfu ya Wapoland kuuwawa.

Ukraine ina matumaini ya kupata ishara za wazi juu ya azma yake ya kujiunga na muungano wa NATO huku Poland ambayo ni moja ya wafuasi wakubwa wa Ukraine ndani ya muungano huo ikisisitiza dhamana ya usalama ya Ukraine.