Rais wa Somalia afuta mkataba wa Somaliland na Ethiopia
7 Januari 2024Matangazo
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesaini sheria kubatilisha mkataba wa jimbo lililojitenga la Somaliland unaoipa Ethiopia uwezo wa kuifikia Bahari ya Shamu kwa mabadilishano wa kutambuliwa jimbo hilo kama taifa huru.
Azma ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuweza kuitumia bahari hiyo imezua msuguano kati ya Ethiopia na majirani zake na kuibua wasiwasi wa kuzuka machafuko mapya katika eneo hilo. Somalia ambayo inaiona Somaliland kama himaya yake, iliyakataa makubaliano hayo yaliyotiwa saini siku ya mwaka mpya.