1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Sudan Kusini amfukuza kazi waziri wa fedha

11 Julai 2024

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfukuza kazi Waziri wa Fedha Awow Daniel Chuong ambae amehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi minne, huku sababu za uwamuzi huo hazikuwekwa hadharani.

https://p.dw.com/p/4i9gl
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Katika miaka ya hivi karibuni, Uchumi wa Sudan Kusini umekuwa ukisuasua, huku kukishuhudiwa kwa changamoto chungumzima ikiwemo ghasia za kikabila, mapato ya mauzo ya mafuta ghafi yakipungua tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2013 hadi 2018, na kutatizika kwa mauzo ya nje kutokana na vita vinavyoendelea katika nchi jirani ya Sudan.

Soma pia:Rais Salva Kiir amfuta kazi waziri wake wa fedha katikati ya mzozo wa kiuchumi

Kiir alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Sudan Kusini mwaka 2011, wakati nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka Sudan. Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi Desemba.