SiasaSyria
Rais wa Syria kuhudhuria mkutano wa kilele Saudi Arabia
18 Mei 2023Matangazo
Rais wa Syria Bashar Assad anaelekea Saudi Arabia kuhudhguria mkutano w akikanda, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta, tangu machafuko yalipoanza Syria mwaka 2011. Hayo yameelezwa na ofisi ya rais.
Assad anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu unaoanza kesho Ijumaa na unaotarajiwa kuidhinisha rasmi kurejeshwa kwa Syria kwenye jumuiya hiyo baada ya kuondolewa kwa miaka 12.
Jumuiya hiyo yenye nchi 22 inatarajiwa kuipokea tena Syria, ambaye rais wake Assad, alialikwa rasmi kuhudhuria, ishara ya kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.
Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria, Saudi Arabia ilikuwa mshirika mkubwa wa makundi pinzani yenye silaha yaliyotaka kumuondoa Assad mamlakani.