Rais Samia athibitisha kuibuka kwa ugonjwa wa Marburg
20 Januari 2025Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, jijini Dar es Salaam.
Amesema majibu ya sampuli zilizochukuliwa kaskazini mwa nchi hiyo, yameonyesha mtu huyo mmoja ameambukizwa ugonjwa huo unaosababisha kifo kwa asilimia 88, ikiwa mtu hatapata tiba.
Wiki iliyopita WHO iiliripoti kile kilichohisiwa kuwa ni maambukizi ya Marburg, ambao ilisema umewaua watu wanane katika mkoa wa Kagera, lakini maafisa wa afya nchini Tanzania waliipinga ripoti hiyo.
Rais Samia amethibitisha leo kwamba vipimo zaidi vimethibitisha kuwepo kwa kesi ya Marburg na sampuli zingine ishirini na tano zilikuwa hasi.
Kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ebola ugonjwa wa Marburg husambaa kwa kugusana kwa karibu na watu wenye ugonjwa huo. Dalili zake ni pamoja na homa, maumivu ya misuli, kuhara na mpaka sasa hakuna chanjo iliyoidhinishwa au matibabu kwa ugonjwa wa Marburg.