Macron asema anazungumza na Bazoum kila siku
2 Septemba 2023Macron amesema hawatambui viongozi wa kijeshi nchini humo na kwamba maamuzi yoyote yatakayofanywa na Ufaransa yatazingatia mazungumzo na Bazoum.
Matamshi hayo ya Rais Macron yalichapishwa katika mtandao wa kijamii wa ikulu ya Elysee ambapo alikuwa akizungumza na wanahabari Kusini mwa Ufaransa kuhusu masuala ya elimu.
Ufaransa yashutumiwa kwa kuingilia masuala ya ndani ya Niger
Katika hatua nyingine, viongozi wa kijeshi nchini Niger, wameishtumu Ufaransa kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo baada ya rais Macron kusisitiza kumuunga mkono Bazoum.
Soma pia:Burkina Faso yaidhinisha muswaada wa kutuma kikosi Niger
Uongozi huo wa kijeshi umesema hayo kupitia taarifa iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa na msemaji wake kanali Amadou Abdramane.