Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan azuru Iraq
22 Aprili 2024Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili nchini Iraq kwa ziara ya kwanza baada ya miaka mingi huku masuala yahusuyo maji, mafuta na usalama wa kikanda yakitarajiwa kuwa ajenda muhimu.
Erdogan amekutana na Rais wa Iraq Abdel Latif Rashid mjini Baghdad na baadae kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mohammed Shia al-Sudani kuhusu hatua za pamoja wanazoweza kuchukua dhidi ya kundi la wanamgambo la PKK, huku akiikaribisha hatua ya Waziri huyo mkuu ya kulitambua kundi hilo kama limepigwa marufuku. Soma:Raia wawili wauwawa Irak katika mashambulizi ya angani ya Uturuki
Waziri Mkuu huyo aidha Raia wawili wauwawa Irak katika mashambulizi ya angani ya Uturukialitangaza makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa na mataifa hayo mawili kwa ajili ya kusimamia usalama, nishati na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo.
Ziara hiyo inafanyika huku mvutano wa kikanda ukiongezeka, ukichochewa na vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi kati ya Israel na Iran.