Rais wa Zamani wa Czech amefariki dunia
18 Desemba 2011Matangazo
Vaclav Havel alifanyiwa upasuaji 1996 kutokana na saratani ya mapafu, na alikuwa akitibiwa ugonjwa unaotokana na shida ya kupumua. Kiongozi huyo alikuwa mmoja kati ya watu muhimu sana katika harakati za Ulaya Mashariki kuupindua mfumo wa siasa za kikoministi na kuja kipindi cha mpito kuelekea demokrasia. Mtunzi huyo maarufu wa michezo ya tamthilia, mpinzani na mwanaharakati wa kuupinga utawala wa kikominsti katika iliokuwa Czechoslovakia, baadae alikuwa rais baina ya mwaka 1989 hadi 1993, na baadae kama mkuu wa jamhuri mpya iloundwa ya Cheki hadi mwaka 2003.
Mwandishi Sudi Mnette