1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Rais wa zamani wa Equador asalimika kuuawa gerezani

6 Januari 2025

Makamu rais wa zamani wa Equador, Jorge Glas, ameokolewa kutoka kwenye gereza alikokuwa amefungwa baada ya jaribio la mauaji dhidi yake.

https://p.dw.com/p/4oqOh
Ecuador Jorge Glas
Makamu wa zamani wa rais wa Equador, Jorge Glas.Picha: JUAN RUIZ/AFP

Mwanasheria wake, Sonia Gabriela Vera, ameituhumu serikali kuhusika na jaribio hilo, huku akiutaka Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati kufuatia mkasa huo kwenye gereza la La Roca.

Kupitia mtandao wa X, wakili huyo amesema mashambulizi hayo yanathibitisha msimamo wao wa muda mrefu kwamba kwa kuwekwa kwenye gereza hilo, serikali ilikuwa imepanga kumuweka kwenye hatari na kumuua kidogo kidogo.

Soma zaidi: Makamu wa zamani wa rais wa Equador alazwa hospitalini

Glas alitiwa nguvuni mwezi Aprili baada ya vikosi vya Equador kuvunja ubalozi wa Mexico mjini Quito, ambako makamu huyo wa rais alikuwa amekimbilia kuomba hifadhi.

Kiongozi huyo ametiwa hatiani kwenye kesi mbili za ufisadi alizoshitakiwa nazo, na bado kuna mashitaka mengine ya ubadhirifu wa fedha za misaada mahakamani.