1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa Ufaransa ahukumiwa kifungo cha miaka 3

1 Machi 2021

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi.

https://p.dw.com/p/3q4Cb
Frankreich | Urteil im Prozess gegen Nicolas Sarkozy
Picha: Michel Euler/AP Photo/picture alliance

Hukumu hiyo iliyotolewa leo na mahakama mjini Paris inajumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje.

Sakorzy alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji mwaka 2014.

Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani kwa kutumia bangili ya umeme. Washtakiwa wenzake wawili ambao ni wakili Thiery Herzog na jaji Gilbert Azibert, pia wamekutwa na hatia na wamehukumiwa kifungo sawa na chake.

Baadae mwezi huu, Sarkozy atakabiliwa na kesi nyingine pamoja na watu wengine 13 kwa mashtaka ya kufadhili kinyume cha sheria kampeni yake ya urais mwaka 2012.