Migogoro
Rais Zelensky atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Poland
15 Januari 2025Matangazo
Kwenye mazungumzo yao watajikita zaidi kutazama namna ya kutatuwa mvutano wa miongo kadhaa kuhusu mauaji ya Wapoland yaliyofanyika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia katika eneo la Volyn ambalo sasa ni magharibi mwa Ukraine.
Zelensky amekuwa akifanya mikutano na mataifa yanayoiunga mkono nchi yake kabla ya rais mteule wa Marekani, Donald Trump hajaingia madarakani.
Soma pia: Mashambulizi ya makombora na droni kutoka Urusi yaitikisa Ukraine
Ukraine ina wasiwasi kwamba serikali ya Trump itailazimisha nchi hiyo kuyakabidhi maeneo yake mengi kwa Urusi ili kumaliza vita vinavyoendelea.
Ziara ya Zelensky Poland pia imekuwa katika kiwingu cha mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Urusi dhidi ya miundo mbinu yake ya nishati.