1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Rais Zelensky afanya mazungumzo na waziri mkuu Donald Tusk

15 Januari 2025

Zelensky amekuwa akifanya mikutano na mataifa yanayoiunga mkono nchi yake kabla ya rais mteule wa Marekani, Donald Trump hajaingia madarakani.

https://p.dw.com/p/4pB2i
Zelensky akutana na viongozi wa Poland huko Warsaw.
Zelensky na waziri mkuu wa Poland Donald Tusk mjini Warsaw.Picha: Radek Pietruszka/PAP/dpa/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwamba kupelekwa kwa wanajeshi wa kigeni nchini Ukraine ni hatua inayoweza tu kuwa sehemu ya hakikisho la kiusalama na haiwezi peke yake kutosheleza usalama wa taifa hilo.

Zelensky ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Warsaw na kuongeza kwamba anapanga kujadili suala hilo la Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer.

Soma pia: Mgogoro wa Ukraine na Urusi: Mashambulizi ya droni, diplomasia ya kimataifa, na mustakabali wa amani

Pia kwenye mkutano huo Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk akiwa pamoja na Zelensky ameahidi kutumia nafasi ya nchi yake kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya, kwa muda wa miezi sita, kusukuma mbele ombi la Ukraine la kutaka uanachama katika jumuiya hiyo.

Zelensky ameitembelea Poland baada ya nchi hizo mbili kufikia makubaliano kuhusu mvutano wa miongo kadhaa juu ya mauaji ya Wapoland yaliyofanywa na wazalendo wa Ukraine, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW