RAMALAH: Baraza jipya la mawaziri laapishwa palestina.
25 Februari 2005Matangazo
Baraza jipya la mawaziri wa Palestina limeapishwa rasmi baada ya waziri mkuu Ahmed Qurei kupata kura ya ndio kutoka kwa wabunge wa chama cha Fatah.
Hapo awali wabunge hao walikataa kuidhinisha orodha ya mawaziri waliochaguliwa na Qurei ambayo iliwapa nafasi zaidi mawaziri wa zamani na kutoa nafasi nne pekee kwa mawaziri wapya jambo ambalo lilizua ubishani mkubwa huku wabunge wa Fatah wakidai kuwa wanapendelea baraza la mawaziri lenye wanasheria wengi dhidi ya wanasiasa wakongwe walioshikilia nyadhfa hizo wakati wa utawala wa Yasser Arrafat.
Wabunge hao wanasema kuwa wana imani na baraza jipya la mawaziri lenye sura mpya 17 katika mawaziri 24 wa Palestina ambao watapiga vita vitendo vya rushwa.