RAMALLAH: Adhabu ya kifo yatekelezwa na wakuu wa Palestina
12 Juni 2005Matangazo
Utawala wa Wapalestina umetekeleza adhabu ya kifo iliyotolewa kwa wafungwa 4.Hatua hiyo imekwenda kinyume na wito wa jumuiya ya kimataifa kuwa adhabu ya kifo ikomeshwe,kama sehemu ya mageuzi yalio muhimu kuunda taifa la Palestina katika siku zijazo.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani,wafungwa 3 walinyongwa na wa nne aliuliwa kwa kupigwa risasi,baada ya kukutikana na hatia ya mauaji.Makundi yanayopigania haki za binadamu yamelaani mauaji hayo na kusema kuwa mashtaka hayakufuata utaratibu wa kisheria unaohitajiwa.Hii ni mara ya kwanza tangu takriban miaka mitatu kuwa adhabu ya kifo imetekelezwa na Wapalestina.