RAMALLAH : Hakuna amani Mashariki ya Kati bila ya taifa la Palestina
15 Mei 2005Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kwamba hakutakuwepo na amani ya Mashariki ya Kati hadi hapo litakapoundwa kwa taifa la Palestina na Jerusalem kuwa mji mkuu wake.
Katika matamshi yake hayo yaliyotangazwa leo hii na vyombo vya habari vya Palestina katika kumbukumbu ya siku mbaya kabisa katika historia yao miaka 57 ya kuanzishwa kwa taifa la Israel Abbas amesema utulivu wa eneo hilo zima unategemea kufanikisha kupatikana kwa makubaliano na ufumbuzi wa haki wa suala la wakimbizi ambapo yeye mwenyewe Abbas akiwa ni mkimbizi.
Maandamano yamefanyika katika maeneo yote ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu kudai haki ya kurudi kwa wakimbizi.
Hatma ya wakimbizi wa asili na kizazi chao ni mojawapo ya masuala nyeti katika mzozo wa Palestina na Israel.