RAMALLAH : Katibu wa bunge la Palestina mbaroni Israel
21 Agosti 2006Jeshi la Israel limemkamata katibu wa Hamas katika bunge la Palestina Mahmoud al Ramahi.
Ramahi ambaye anashikilia nafasi ya nne ya juu katika bunge la Palestina alikamatwa nyumbani kwake huko El-Bireh mji ulioko karibu na Ramallah.Msemaji wa Israel amethibitisha kukamatwa kwa afisa huyo.
Ramahi anakuwa afisa wa karibuni kabisa katika mfululizo wa viongozi waandamizi wa Hamas wakiwemo mawaziri wanaotiwa mbaroni na Israel kufuatia shambulio la wanamgambo wa Kipalestina waliovuka mpaka katika Ukanda wa Gaza na kuuwa wanajeshi wawili wa Israel na kumteka nyara mmoja.
Kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja siku moja baada ya wanajeshi wa Israel kumkamata naibu waziri mkuu wa Palestina na mwanachama mwandamizi wa Hamas Nasser al Shaer.