RAMALLAH: Polisi wa Palestina wawatawanya watu kati ya mpaka wa Gaza na Misri
18 Septemba 2005Matangazo
Polisi wa Palestina wamelazimika kufyatua risasi angani kuutawanya umati wa watu waliokuwa wakiwarushia mawe kati ya mpaka wa ukanda wa Gaza na Misri. Tukio hilo limefanyika wakati polisi walipokuwa wakijaribu kuwazuia watu kuvuka mpaka. Kuanzia mwanzo wa juma hili, watu wengi wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia kwenye eneo hilo tangu Israel ilipoondoka ukanda wa Gaza.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameapa kuzuia watu kuvuka mpaka na kuingia kwenye eneo hilo. Mamlaka ya Palestina imesema tayari imewatuma askari 1,500 kulifunga eneo hilo.