1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Rais wa Palestina kukutana na waziri mkuu wa Israel.

11 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDW

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema yuko tayari kukutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert haraka iwezekanavyo ili kurejea tena katika majadiliano.

Abbas alikuwa akizungumza baada ya kukutana mjini Ramallah na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ambaye analizuru eneo la mashariki ya kati.

Siku ya Jumamosi , Olmert amesema yuko tayari kuwa na mazungumzo bila masharti na Abbas na ameliambia baraza la mawaziri la Israel kuwa huu ni wakati wa kujenga upeo mpya na Wapalestina.

Blair amesisitiza umuhimu wa Wapalestina kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambao utatambua kuwapo kwa taifa la Israel na kukana sera za utawala unaoongozwa na chama cha Hamas. Blair anatarajiwa kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora mjini Beirut leo.