1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Viongozi wa Palestina washindwa kuafikiana juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvF

Rais wa Palestina, Mahmud Abbas kutoka chama cha Fatah na waziri wake mkuu, Ismail Haniya kutoka chama cha Hamas,walishindwa kuondoa tofauti zao kuhusu uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Miongoni mwa matatizo yaliojitokeza ni pamoja na nani ataiongoza serikali hiyo iwapo itaundwa. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana tena leo kwa mazungumzo zaidi juu ya swala hilo.

Wakati hayo yakiarifiwa, majeshi ya Israeli yameondoka kutoka mji wa kaskazini mwa ukanda wa Gaza wa Beit Hanun baada ya operesheni ya wiki nzima ambapo kwa uchache wapalestina 50 waliuawa na mia kadhaa kujeruhiwa.