RAMALLAHCondolezza Rice kukutana na Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas
23 Julai 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice hii leo atafanya mkutano na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas huko magharibi mwa ukanda wa ghaza.
Mkutano huo unatazamiwa kutuwama juu ya suala la kuwepo utulivu wakati wa kutekelezwa kwa mpango wa Israel wa kuyahama maeneo ya wapalestina.
Hapo jana bibi rais alisema atasisitiza katika mkutano huo wa leo haja ya kuzuiwa kwa juhudi za magaidi za kutaka kuyaharibu matumaini ya wapalestina ya kurejeshewa ardhi yao na waisrael.
Mpango wa Israel wa kuyahama maeneo ya wapalestina umepangiwa kuanza agosti 17 lakini baadhi ya waisrael wanaupinga mpango huo.