RAMALLAH:Kura´ya kuidhinisha baraza jipya la mawaziri yahairishwa,Palestina
23 Februari 2005Wanamageuzi nchini Palestina wamemlazimisha waziri mkuu Ahmed Qurei kufikiria kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri. Kura iliyokuwa ikitarajiwa kupigwa bungeni ili kuidhinisha baraza jipya la mawaziri jumatatu ,imehairishwa hadi Alhamisi kufuatia wanasheria kutaka wajumbe wapya zaidi na wanamageuzi na kupunguzwa wajumbe wazamani waliokuwa wakiongozwa na Marhum Yasser Arrafat.
Taarifa zimeleza kuwa baraza hilo limeonekana kutawaliwa na Ufisadi.Duru zimearifu katika mabadiliko yatakayofanywa na Qurei katika Baraza hilo huenda kukawepo nyuso za watu wapya ikilinganishwa na orodha yake ya zamani ambayo ilikuwa na watu wanne wapya.Anatarajiwa kuwajumuisha ndani wafuasi wa Arrafat kama vile Nabil Shaath ambaye anakisiwa kuwa makamu wa waziri mkuu,na Saeb Erekat.