Ramaphosa akabiliwa tena na mchakato wa kumuondowa
4 Oktoba 2024Kesi hiyo itakayoanza kusikilizwa mwezi Novemba inahusu kufichwa kitita cha dola 500,000 za Kimarekani kwenye makaazi yake ya shamba na kisha baadaye fedha hizo kuibiwa na wezi.
Ramaphosa aliepuka kupigiwa kura ya kuondolewa madarakani mwaka 2022 baada ya chama chake cha African National Cogress (ANC) kutumia wingi bungeni kuzuia hoja hiyo kuwasilishwa.
Soma zaidi: Raia nchini Afrika Kusini waanza kupiga kura ya mapema chini ya kiwingu cha usalama duni
Hatua hiyo ilichukuliwa licha ya uchunguzi huru uliofanywa kuonesha kiongozi huyo alikuwa na maswali ya kujibu kuhusu matendo yake na kupendekeza kufanyike uchunguzi mpana zaidi juu ya kashfa hiyo.
Shinikizo dhidi ya Ramaphosa lilikuwa limepungua tangu chama chake kilipofikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na vyama kadhaa vya upinzani.
Lakini vyama vya EFF na ATM, ambavyo havimo kwenye serikali, EFF na ATM, vimewasilisha maombi mbele ya mahakama ya katiba kwa hoja kwamba bunge lilishindwa kutimiza jukumu lake la kikatiba la kumwajibisha rais wa nchi hiyo.