SiasaAfrika Kusini
Ramaphosa apigia debe umoja baada ya matokeo mabaya ya ANC
3 Juni 2024Matangazo
Ramaphosa ameyasema haya baada ya chama chake cha African National Congress, ANC, kupoteza wingi wake wa miaka 30 bungeni katika uchaguzi mkuu nchini humo.
Lakini katika kile kinachoashiria msukosuko unaotarajiwa siku chache zijazo, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyechafuliwa na tuhuma za ufisadi Jacob Zuma, alisusia hafla ya kutangazwa kwa matokeo na chama chake kimekataa kuyatambua.
Hesabu za mwisho zimeonesha chama cha ANC kimepata viti 159 kati ya 400 katika bunge la nchi hiyo, kikifuatiwa na Democratic Alliance kilichopata viti 87 na uMkhonto weSizwe cha Zuma kilichopata viti 58.