1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya CIA kuhusu mashambulio ya kigaidi ulimwenguni

28 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIZ

Ripoti iliyotangazwa na idara ya upelelezi ya Marekani CIA inasema mashambulio 650 ya kigaidi yamefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kote ulimwenguni na kugharimu maisha ya zaidi ya watu 1900.Ripoti hiyo inasema zaidi ya nusu ya mashambulio hayo ya kigaidi yametokea kusini mwa bara hindi.Kitovu cha mashambulio hayo ni katika eneo la Kashimir linalogombaniwa na India na Pakistan.Idadi kubwa zaidi ya wahanga imeirpotiwa mashariki ya kati ambako watu 726 wameuwawa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Marekani inazitaja Cuba,Iran;Libya,Korea ya kaskazini,Sudan na Syria kua nchi zinazowaunga mkono magaidi.Ripoti ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imeorodhesha makundi 40 kua ni ya kigaidi,miongoni mwao yanakutikana Hisbollah na Hamas.Ripoti hiyo inaitaja Irak kua ni kitovu cha mapambano dhidi ya ugaidi.