1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya uchunguzi: Mahsa alikufa kwa magonjwa mengine

7 Oktoba 2022

Ripoti ya mchunguzi wa vifo vya ghafula nchini Iran imesema Mahsa Amini hakufa kutokana na kipigo kichwani, miguuni na mikono lakini kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa viungo mbalimbali mwilini.

https://p.dw.com/p/4HuU6
Frankreich | Solidarität für iranische Demonstranten in Paris
Picha: Aurelien Morissard/AP/picture alliance

Ripoti hiyo imesema kifop cha msichana huyo wa Kikurdi  kimesababishwa na upungufu wa oksijeni inayoingia kwenye ubongo kitaalamu "hypoxia". 

Kwa mujibu wa ripoti rasmi iliyotolewa na shirika la habari la serikali IRNA, ripoti hiyo haikusema kama alikuwa na majeraha yoyote lakini ilisema alianguka akiwa kizuizini kutokana na magonjwa aliyokuwa nayo.

Aidha ripoti hiyo inasema kwamba kutofanya kazi vyema kwa mfumo wa moyo kupumua ndani ya dakika za kwanza alipata upungufu wa oksijeni na kusababisha uharibifu wa ubongo.

soma Ni ipi kazi ya Polisi wa maadili wa Iran?

Wakili wa familia ya Amini, Saleh Nikbakht, hapo awali aliiambia tovuti ya habari ya Etemadonline kwamba "madaktari wanaoheshimika" wanaamini kuwa alipigwa chini ya ulinzi.

soma Khamenei azishtumu Marekani na Israel kwa machafuko Iran

Polisi wamekanusha kwamba alipata madhara akiwa kizuizini lakini awali walisema alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kupelekwa kituoni kwa kile walichokitaja kama "kuelimishwa".

Familia ya msichana huyo imekanusha kwamba alikuwa na matatizo yoyote ya moyo.

Wabunge wa Ubelgiji waonyesha mshikamano

Schauspielerin Juliette Binoche schneidet sich Haare |  Protest gegen Iran
Muigizaji Juliette BinochePicha: SOUTIENFEMMESIRAN/INSTAGRAM/REUTERS

Huku haya yakijiri Waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Hadja Lahbib na wabunge wengine wawili walinyoa nywele zao bungeni, katika mshikamano na maandamano dhidi ya serikali nchini Iran .

Hii ni baada ya naibu wake Darya Safai mzaliwa wa Iran kukata nywele zake bungeni baada ya kumuuliza waziri kuhusu hatua ya Ubelgiji kukabiliana na ukandamizaji wa waandamanaji ndani ya Iran. Mbunge Goedele Liekens pia alikata nywele zake.

Lahbib, mzaliwa wa Ubelgiji na wazazi wa Algeria, aliliambia bunge kwamba serikali yake itaomba Umoja wa Ulaya kulazimisha vikwazo dhidi ya wahusika wa ukandamizaji wakati mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo watakapokutana baadaye mwezi huu.

Idadi ya vifo yaongezeka

Iran Proteste nach dem Tod von Mahsa Amini
Picha: NNSRoj

Hasira juu ya kifo cha Mahsa Amini imesababisha wimbi kubwa zaidi la maandamano nchini Iran katika muda wa karibu miaka mitatu na ukandamizaji ambao umeua makumi ya waandamanaji na wengine wengi kukamatwa.

soma Zaidi ya 75 waandamanaji wauawa Iran

Wasichana wengine wadogo pia wamepoteza maisha kwenye maandamano hayo, lakini shirika la kutetea haki za binaadam la Amnesty International linasema Iran imekuwa ikilazimisha familia zao kukiri kwenye televisheni kwamba serikali haijaahusika.

Taarifa ya shirika la haki za binadamu la Amnesty International wiki moja iliyopita, ilisema kuwa Iran imekuwa ikitumia nguvu kupita kiasi ili kusitisha maandamano yanayoongozwa na wanawake. Ilisema imepata hati iliyotolewa kwa makamanda wa vikosi vya jeshi katika majimbo yote mnamo Septemba 21 ikiwaamuru "kukabiliana vikali" na waandamanaji.

soma Raisi aonya waandamanaji nchini Iran

Uvujaji mwingine wa hati ulionyesha kamanda katika jimbo la Mazandaran aliviamuru vikosi "kukabiliana bila huruma, hadi kusababisha vifo, machafuko yoyote ya waasi na wanaopinga mapinduzi".